Tuesday 2 February 2016

Mbunge Joseph Msukuma Kasheku Ataka Serikali Ihalalishe Bhangi na Mirungi Kama ilivyohalalisha Viroba


Mbunge  wa  Geita vijijini kwa tiketi  ya  CCM, ndugu Joseph Kasheku (Msukuma)  ameishauri serikali  kuruhusu kisheria kilimo cha Bhangi na Mirungi  ili kuiwezesha  kujipatia  fedha za kigeni  kutokana  na  mauzo  ya  mazao hao

Mbunge huyo aliyasema hayo jana katika kikao cha 5 cha bunge la 11 linaoendelea na vikao vyake katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma.

''Mheshimiwa mwenyekiti zao la mirungi na bhangi kuna nchi zinaruhusu .Mfano mzuri mfano ni majirani zetu wa Kenya ambao ndege mbili kubwa hutua nchini humo kuchukua mirungi na kupeleka ulaya,sasa kwa nini sisi tusiendeleze zao hili linalopatikana Geita na maeneo ya Bunda mkoani Mara na maeneo mengine nchini ili wananchi wanufaike kwa kuuza zao hilo ?'' Alihoji Msukuma na kuongeza;

"Kwa wasukuma kule kwetu mtu akitumia bhangi anapata nguvu ya kulima sana hata hekari mbili lakini inakatazwa na wakati huo huo vijana wetu  tumewaruhusu kutumia viroba ambavyo huwadhoofisha sana pengine kushinda hata bhangi, naomba tufanye utafiti upya juu ya hili.

"Wapo wenzetu humu (wabunge) wanaitumia bhangi na hakuna madhara yoyote, tena wanachangia hoja kwa ufasaha kabisa."

Baada  ya hoja hiyo ya Mbunge Msukuma, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt Khamis Kigwangalla alisimama kumjibu ambapo alisema madawa ya kulevya aina ya bhangi na mirungi yana athari kubwa sana za kiafya na hasa afya ya ubongo .

Kingwangalla alisema serikali kwa namna yoyote haitakubali kuruhusu au kujadili  kuhalalishwa kwa madawa hayo.

No comments: