Sunday 21 February 2016

Mwanasheria Jijini Mbeya awaangukia madiwani ili wakubali kupitisha kifungu cha bajeti ya kumnunulia suti kila mwezi yenye thamani ya Tsh. 500,000.



Madiwani wa Halmashauri ya Mbeya vijijini wamegoma kupitisha kifungu cha bajeti ya kumnunulia mwanasheria wa halmashauri suti ya Tsh. 500,000 kila mwezi.

Awali akiwakilishabajeti ya mwaka 2016/2017 kwenye Baraza la Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri Mbeya Vijijini, Mwanasheria Prosper Msivala alisema kila mkuu wa idara atapata Tsh. 180,000 kwa ajili ya mawasiliano huku wanasheria wakipewa sh. 500,000.

Msivala alisema suti ya mwanasheria ni pamoja na viatu, shati, suruali na koti pamoja na skafu yake

Diwani wa Maendeleo Mbeya Vijijini, Daniel Mwanyamale alipinga mwanasheria kushonewa sare kila mwezi kwa sh500,000

Aliwataka waandaaji wa bajeti hiyo kuangalia upya suala hilo na kwamba hata suala la kupewa sh. 180,000 za mawasialiano litazamwe upya kwani halikubaliki

Diwani Ramadhi Jelambaa alisema afadhali feza hizo zipelekwe kwenye shughuli za maendeleo ukiwamo ujenzi wa madarasa na ununuzi wa dawa za vituo na zahanati

Hata hivyo Mwanasheria Msivala alitetea fedha hizo akisema ni jukumu la halmashauri kutoa na kuwaomba madiwani wapitishe bajeti hiyo

“Ndugu zangu kila mwanasheria anapoajiriwa katika halmashauri yetu ni lazima kila mwanasheria apate sh500,000 na hilo lipo kisheria,” alisema Msivala

Ikumbukwe wakati hilo liki jiri la baraza la madiwani kupinga kupitisha kifungu cha bajeti ya mwanasheria kununuliwa suti inayoghalimu kiasi cha sh,500,00 kila mwezi huku madiwani wakipewa kiasi cha sh.180,000 kwa mwezi kwa ajili ya mawasiliano. 

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amekua akisisitiza matumizi mazuri ya fedha za umma huku akiwa wajibisha haraka iwezekanavyo baadhi ya viongozi wanaothibitika kutumia vibaya fedha za umma, 

No comments: