Na Ester Macha,Mbeya.
MAMLAKA
ya majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya, imesema kuwa shule
za serikali pamoja na jeshi la polisi ndizo zinaongoza kwa kuwa na
madeni ya makubwa ya maji kutokana na kutolipwa kwa wakati na hivyo
kusababisha mamlaka kuwa na utendaji mgumu wa kazi .
Kufuatia
kuwepo kwa madeni hayo mamlaka ya maji imeanza opareshemni ya kukata
maji kwa maeneo yote ya wananchi ambako hawajalipa ada.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya maji Jijini hapa
Bibi. Neema Stanton wakati alipozungumza na gazeti hili ofisini kwake
kuhusu ulipaji wa madeni ya maji kwa taasisi za serikali ,makampuni
binafsi pamoja na wananchi.
“Kwenye
huu ulipaji wa madeni ya maji kwakweli hizi taasisi za serikali
zimekuwa ni tatizo kubwa kwa upande wa madeni licha ya kuwa mamlaka
bado inaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa madeni hayo yanalipwa
mapema”alisema.
Akizungumzia
kwa upande wa shule za sekondari za serikali Bi.Stanton alisema nazo
zimekuwa zikisuasua kwa kiasi Fulani kutokana na wao kuweka kipaumbele
mambo Fulani kwenye shule zao.
Hata
hivyo Ofisa Uhusiano huyo alisema kwa upande wa shule za sekondari za
binafsi wao wamekuwa wepesi wa kulipa madeni lakini kwa kufuatiliwa
sana na mamlaka ndipo wanalipa madeni hayo.
“Lakini
pia licha ya kuwa wanalipa lakini ni wajibu wao kutakiwa kulipa kwa
wakati bila kufuatwa kwani kulipa ni wajibu wao sababu wanatumia maji
isitoshe kwa suala la shule ambalo ni muhimu zaidi”alisema.
Aidha
Bibi.Stanton alitoa wito kwa shule za serikali kuweka kipaumbele
ulipaji wa bili za maji kwani fedha hizo zinasaidia malipo ya
umeme,madawa kwenye maji ambayo yanatumia grama kubwa.
“Kwa ujumla grama za uendeshaji ni nyingi hivyo ni vema shule na taasisi za serikali zikatambua umuhimu wa huo “alisema.
Hata
hivyo Ofisa uhusiano huyo alipotakiwa kuzungumzia kiasi kamili cha
madeni ambayo mamlaka ya maji inadai alisema suala hilo lipo kwa meneja
ambaye ndiye ana takwimu sahihi.
No comments:
Post a Comment