UP DATE YA AJALI MBALIZI MBEYA.. MBUNGE DR.MWANJELWA ANUSURIKA KUFA
HII NDIYO GARI ALIYOKUWEMO MBUNGE MARY MWANJELWA, HAPA NI MBALIZI IKIWA IMETEKETEA KWA MOTO.
· Ajali
mbaya yatokea Mbalizi Mbeya
· Katibu
wake ateketea kwa moto, ni zaidi ya watu watano
Na, Gordon
Kalulunga, Mbeya
MBUNGE wa viti maalum mkoani Mbeya kupitia tiketi ya Chama
cha Mapinduzi (CCM) Dr. Mary Mwanjelwa, amenusurika kufa katika ajali mbaya
iliyotokea jana eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa baada ya
gari lake kugongwa na kuteketea kwa moto.
Ajali hiyo imehusisha magari Manne likiwemo Lori la Mafuta
kampuni ya lake Oil lenye namba za usajili T 814 BTC , gari ndogo ya abiria
(Hiace) yenye namba za usajili T 299 BCE na gari ya Mbunge huyo Mary Mwanjelwa
Toyota Hilux T 671 ABM
Watu zaidi ya saba walifariki papo hapo huku wengine miili
yao ikiwa imeteketea vibaya kwa mota baada ya gari hizo kugongana kisha
kulipuka.
Mashuhuda wa ajali hiyo wakiwemo majeruhi, walisema Petro
Tank iliyokuwa imebeba mafuta, iliferi breck katika mteremko wa Mlima Iwambi
kisha kuliparamia Lori lingine na kuigonga gari ya Mbunge Mwanjelwa kisha
kuvaana uso kwa uso na gari ya abiria iliyokuwa ikitokea eneo la Mbalizi.
kalulunga blog kilishuhudia mtu aliyeongoza uokojai ambapo alikuwa ni Koplo Mathias Joachim wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania 44
KJ Mbalizi Mbeya Karume Camp.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alifika eneo la tukio
na ametoa pole kwa wafiwa kisha ameelekea Hospitali ya Ifisi Mbalizi kwa ajili
ya kuwajulia hali majeruhi akiwemo Mbunge huyo.
Mbunge Mary Mwanjelwa, akiwa Hospitalini hapo alimshukuru
Mungu kwa kumnusuru kisha akauliza kama dereva wake anayejulikana kwa jina la
Rajab na katibu wake Muhtasi Amina ambapo aliambiwa kuwa wapo Hospitali ya Rufaa
ya Mbeya.
Dereva wake Mr. Rajabu ambaye alipelekwa katika Hospitali
hiyo ya Ifisi, ameumia vibaya kichwani na miguu yote miwili huku katibu wa
Mbunge huyo imesemekana kuwa amekufa kwa kuteketea kwa moto ndani ya gari hiyo.
Kati ya zaidi ya watu saba ambao wamefariki katika ajali
hiyo yumo askari Polisi wa kituo kidogo cha Mbalizi aliyetajwa kwa jina la PC
Samson.
Kikosi
kazi cha mtandao huu wa kalulunga.blogspot.com kinatoa pole kwa wafiwa
wote na Mungu awasaidie majeruhi wapone haraka kwa ajili ya kuendelea
kulijenga Taifa letu la Tanzania.
HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI
HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA
FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO
ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKA ENEO LA TUKIO AMBAPO MAGARI HAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATU KUMI.
WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI
HUU NDIO MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE
HAYA NI MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALO LILIUNGUA LOTE
WANANCHI MBALI MBALI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA WALIO PATA AJALI
No comments:
Post a Comment