Tuesday, 25 June 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI





“PRESS RELEASE” TAREHE 25. 06. 2013.


WILAYA YA RUNGWE - MAUAJI

 

MNAMO TAREHE 24.06.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. SAITA D/O MBONA,MIAKA 65,KYUSA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA SUMA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.  MAREHEMU ALIKUWA ANAISHI PEKE YAKE ALIJERUHIWA KWA  KUKATWA MAPANGA KICHWANI USIKU WA TAREHE 22.06.2013 BAADA YA KUVAMIWA NYUMBANI KWAKE  KIJIJI CHA SUMA AKIWA AMELALA. CHANZO NI MZOZO WA MUDA MREFU WA KUGOMBEA MASHAMBA. WATUHUMIWA WAWILI 1.SALUM S/O MWAMBONA, MIAKA 45, KYUSA, MKULIMA NA 2.FEDA D/O BUSILA KYUSA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ITAGATA WAMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUTATUA KERO/MATATIZO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO AU KUFUATA SHERIA.

 

WILAYA YA MBEYA MJINI - AJALI YA GARI KUWAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU NA
                                                      KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.

 

MNAMO TAREHE 25.06.2013 MAJIRA YA SAA 23:00HRS HUKO NJIA PANDA ILOMBA BARABARA YA MBEYA/IRINGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA AINA YA TOYOTA L/CRUISER HARDTOP LILIWAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU WATANO NA KUSABABISHA KIFO KWA VEDASTO S/O EMANUEL,MIAKA 20,MSAFWA,MKAZI WA MWANJELWA.AIDHA WATU WALIOJERUHIWA  KATIKA TUKIO HILO NI 1. LUSAJO S/O JOHN, MIAKA 22, MKINGA, 2. YOHANA S/O DAUDI, MIAKA 20, KYUSA, 3. HUSEIN S/O MBILINYI,MIAKA 20,MKINGA WOTE WAKAZI WA MWANJELWA AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA 5. ANDREW S/O DAUD, MIAKA 20, KYUSA, MKAZI WA MWANJELWA AMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI.  CHANZO KINACHUNGUZWA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA  PAMOJA NA GARI  LAKE.

 

WILAYA YA KYELA -  KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

 

MNAMO TAREHE 24.06.2013 MAJIRA YA SAA 22:30HRS HUKO ENEO LA MBUGANI KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO HARIRI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MISAKO WALIWAKAMATA 1. HAPIPE S/O CHIZUKA, MIAKA23,MNGONI,MKULIMA NA 2.WATSON S/O TEMBO,MIAKA 30,MNGONI WOTE NI RAIA NA WAKAZI WA MZUZU NCHINI MALAWI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI .  MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI HATUA ZA HARAKA ZICHUKULIWE DHIDI YAO IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.

No comments: