Shughuli imekamilika: Wachezaji wa Brazil wakiinua Kombe la Mabara baada ya kuwafunga mabingwa wa dunia, Hispania
Sema hureee: David Luiz akiwa na Kombe baada ya sherehe Maracana
Nyota wa mchezo: Neymar ameanza kupata mafanikio kimataifa
Mwimbaji wa Colombia, Shakira alikuwepo Rio kumuangalia mpenzi wake, Gerard Pique akiichezea Hispania
IMEWEKWA JULAI 1, 2013 SAA 9:05 USIKU
BRAZIL
imetwaa Kombe la Mabara baada ya kuifunha Hispania mabao 3-0 kwenye
Uwanja wa Jornalista Mario Filho (Maracana) mjini Rio de Janeiro,
Brazil.
Katika mchezo huo, mabingwa wa Dunia na Ulaya walipoteza mchezaji mmoja na pia wakashindwa kufunga kwa penalti.
Shukrani
kwao Fred aliyefunga mawili, la kwanza dakika ya pili na la tatu dakika
ya 47 kwa pasi ya Hulk na Neymar aliyefunga la pili dakika ya 44 kwa
pasi ya Oscar.
Dakika ya 68, Pique alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mchezaji mwenzake mpya wa Barcelona, Neymar.
Dakika
ya 54 Marcelo alimuangusha kwenye eneo la hatari Navas, lakini Sergio
Ramos akakosa penalti baada ya mkwaju wake kuota mbawa.
Kikosi
cha Brazil kilikuwa: Julio Cesar; Dani Alves, Thiago Silva (capt),
David Luiz, Marcelo; Oscar, Luiz Gustavo, Paulinho/Hernanes dk 88;
Fred/Jo dk80, Neymar, Hulk/Jadson dk73.
Hispania:
Iker Casillas; Alvaro Arbeloa/Azpilicueta dk46, Gerard Pique, Sergio
Ramos, Jordi Alba; Xavi, Sergio Busquets, Andres Iniesta; Juan
Mata/Navas dk 52, Fernando Torres/Villa dk 59 na Pedro.
Mkombozi: Fred amefunga mawili
Pata picha itakuwaje Lionel Messi atakapoanza kucheza pamoja na Neymar
Kwaheri: Gerard Pique akionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumuumiza Neymar aliyelala chini
Penalti ya Sergio Ramos iliota mbawa
Mechi imaisha? Fred akishangilia bao lake la pili na la tatu kwa Brazil
Kazi ya ziada: David Luiz aliokoa kwenye mstari wa goli shuti la Pedro, ambalo kama lingeingia ingekuwa 2-1
Neymar akifumua kumtungua Iker Casillas na kufanya 2-0
Shangwe tu: Neymar akiwarukia mashabiki Maracana
Kijana
mwenye bahati: Alvaro Arbeloa angepewa kadi nyekundu kwa rafu
aliyomchezea Neymar - wachezaji hao walikuwa peke yao wakati wa mapumzi
beki huyo wa Real Madrid alipomuangusha mwenzake
FFU wa Brazil: Polisi wa kutuliza ghasia wakipuliza gesi ya moto kudhibiti fujo nje ya Uwanja wa Maracana
Fred akifunga
Fred alifunga dakika ya pili tu bao la kwanza
Mwanzo mzuri: Fred akishangilia na Neymar
No comments:
Post a Comment