London,
England
MSHAMBULIAJI
wa Napoli, Edinson Cavani amemalizana na Chelsea, baada ya kukubaliana maslahi
yake binafsi ya kujiunga na klabu hiyo majira haya ya joto.
Vyombo
vya habari nchini Italia, vimeeleza kuwa Cavani amekubali kulipwa mshahara
kiasi cha pauni milioni 7.2 kwa mwaka, lakini sasa itambidi kuishawishi Napoli
kushusha ada yake ya uhamisho ili zoezi hilo likamilike.
Chelsea
haipo tayari kulipa euro milioni 63 ambazo ni sawa na pauni milioni 53
zinazohitajika na Napoli, ili kuvunja mkataba wake, hivyo Cavani itabidi
amshawishi Rais wa klabu hiyo, Aurelio de Laurentiis kushusha dau hilo.
Napoli inataka kumtwaa Ramires pamoja na fedha kama sehemu ya kukubali kumwachia Cavani, lakini Chelsea haipo tayari kuachana na Mbrazil huyo.
No comments:
Post a Comment