|
baada ya ajali hiyo, |
|
Inavyoonekana kwa nyuma
|
|
hii ni sehemu ya mbele ya gari hilo |
|
Scania lililogongwa kwa nyuma |
|
Sehemu ambayo gari hilo dogo liliingia |
AJALI mbaya
iliyohusisha gari dogo aina ya Land Rover Freelander lenye namba T368
CVK na roli la mizigo aina ya Scania lenye namba T346 BRF imetokea usiku
wa juzi katika eneo la Lugemba, kilomita kadhaa kabla ya kufika mji wa
Mafinga.
Taarifa za awali
zinaonesha kwamba dereva wa gari hilo jina lake bado halijapatikana
alifariki papohapo baada ya gari yake kuingia nyuma ya roli hilo
lililokuwa limepaki kandakando ya barabara ya Mafinga Dar es Salaam,
akiwa katika mwendo mkali.
Mwanafunzi wa
kike wa Chuo Kikuu cha Tumaini aliyekuwemo katika gari hilo amenusurika
kufa; binti huyo ambaye pia jina lake halikupatikana amelazwa katika
hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya ikiwa ni
pamoja na kukatika mkono.
Mashuhuda wa
tukio hilo wamesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 3 usiku. Na baada
ya ajali hiyo wasamalia wema waliukumbiza mwili wa marehemu na majeruhi
katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.
Jeshi la Polisi
limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na taarifa za awali zinaonesha
dereva wa gari hilo alikuwa amelewa wakati akiendesha gari hilo.
No comments:
Post a Comment