Thursday, 3 July 2014

HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA YAKABIDHIWA VYANDARUA 100.


ASKOFU wa TAG Jimbo la Mbeya Kaskazini, Dk. Donald Mwanjoka akiwakabidhi vyandarua 100 viongozi wa Hospitali ya mkoa Mbeya

ASKOFU wa TAG Jimbo la Mbeya Kaskazini, Dk. Donald Mwanjoka akihutubia katika hospitali ya mkoa Mbeya

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina akimkaribisha mgeni rasmi

Dr. Leonard Maboko Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ya TAG ambae pia ni Mkurugenzi wa NIMR, akitoa neno kwa wageni

Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya mkoa Mbeya wakimsikiliza mgeni rasmi


Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dk. Gloria Mbwile, Alilipongeza Kanisa kwa kutimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania pamoja na kutambua umuhimu wa huduma za jamii.






ASKOFU wa TAG Jimbo la Mbeya Kaskazini, Dk. Donald Mwanjoka amekabidhi vyandarua 100 katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya jubilee ya miaka 75 ya kuanzishwa kwa kanisa hilo.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi vyandarua hivyo, Askofu huyo alisema zoezi hilo linafanyika kutokana na Kanisa hilo kitaifa kuanzishwa Mkoa wa Mbeya pamoja na sherehe kufanyika kitaifa Mkoa wa Mbeya.
Awali akitoa utambulisho katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii wa TAG, Dk. Leonard Maboko, ambaye pia ni Mkurugenzi wa NMR, alisema mbali na askofu huyo kukabidhi vyandarua hivyo katika hospitali hiyo pia Maaskofu wengine wametawanyika katika Hospitali za Jiji la Mbeya na Wilaya ya Mbeya kwa ajili ya kukabidhi vyandarua hivyo.
Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dk. Gloria Mbwile, Alilipongeza Kanisa kwa kutimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania pamoja na kutambua umuhimu wa huduma za jamii.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina aliwashukuru Kanisa kwa msaada na kuongeza kuwa kitendo hicho ni kutekeleza mfumo wa serikali wa kuzishirikisha sekta binafsi katika mfumo wa (PPP).
Aliongeza kuwa hivi sasa serikali inakabiliwa na kutekeleza mpango wa mileniawa kupunguza vifo vya mama na mtoto kutokana na Malaria hivyo kitendo cha Kanisa kutoa msaada huo ni kuisaidia Serikali kwa kutoa vyandarua bure tofauti na serikali ya kutoa kwa mfumo wa hati Punguzo.

No comments: