TIMU za Tanzania Prison na Mbeya City zote za jijini Mbeya zinatarajia kupimana nguvu katika mtanange utakaopigwa jumamosi hii(Julai 5, mwaka huu) kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini hapa.
Aidha mchezo huo wa kirafiki pia ni maalumu kwa ajili ya majaribio ya mfumo mpya wa kielektroniki wa mashabiki
kuingia uwanjani kwa kulipia tiketi zao kupitia mitambo maalumu
iliyofungwa katika Uwanja huo na baadhi ya viwanja vitakavyotumika
katika msimu ujao wa ligi kuu.
Hayo
yalibainishwa jana katika Semina elekezi iliyotolewa kwa Waandishi wa
Habari Mkoa wa Mbeya na viongozi wa mpira wa miguu iliyotolewa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) ikiongozwa na Msemaji wake Bonifasi
Wambura iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine.
Akizungumza
katika Semina hiyo Mwezeshaji ambaye ni mtaalamu wa mitambo hiyo kutoka
benki ya CRDB, Kurrington Chahe, alisema tiketi za mchezo huo zilianza
kuuzwa siku tano kabla na ndivyo itakavyokuwa katika michezo yote ya
ligi kuu.
Alisema
lengo ni kumfanya shabiki kununua tiketi popote alipo hapa nchini
kutokana na mfumo huo kufanyika kwa nia ya mtandao ambapo shabiki
anaweza akanunua kwa njia ya mitandao ya simu ama kufika katika tawi la
Benki ya CRDB.
Aliongeza
kuwa lengo la kufunga mashine hizo ni kudhibiti mapato ya uwanjani
ambapo fedha zote zitakuwa zikipitia moja kwa moja benki na kwa mawakala
na sio mikononi mwa watu kama ilivyokuwa awali.
Alisema
kutumika kwa mfumo huo pia kutaondoa wanaojiita stafu ili wapiti bure
pamoja na makomandoo wa timu wanaokaa milangoni na kuingiza watu bure.
Kwa
upande wake Afisa Habari wa TFF, Bonifasi Wambura alisema mfumo huo ni
mpya na unaweza ukawa na changamoto nyingi ndiyo maana wameandaa mechi
ya kirafiki baina ya Mbeya city na Tanzania Prison ili kujaribu matumizi
ya mitambo hiyo.
Alisema
kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa shilingi 3000 ambapo shabiki
atafika na tiketi yake getini ambayo itaskaniwa kwenye mashine ili
kubaini idadi ya watu wakaoingia uwanjani pamoja na mapato yake ambapo
alisema utaratibu huo utaondoa usumbufu wa kuanza kuhesabu mapato baada
ya mechi.
Wambura
alisema tiketi zitasitishwa kuuzwa katika kipindi cha pili cha mchezo
kinapoanza ili kuweza kurahisisha utaratibu mwingine kufanyika ambapo
aliongeza kuwa mfumo huo utapunguza gharama nyingi zikiwemo magari ya
kuuzia tiketi.
Katika
mchezo huo Mawakala zaidi ya 15 wamefundishwa na kuteuliwa kuuza tiketi
hizo kutoka Wilaya za Mkoa wa Mbeya na jijini hapa.
No comments:
Post a Comment