BAADHI ya wazee kutoka tarafa za unyakyusa na ntebela
wilayani Kyela mkoani Mbeya wamemtaka mwenyekiti mtendaji wa asasi ya pambana
saidia jamii wilayani humo Abraham Mwanyamaki kujipanga kuchukua mikoba ya
mbunge wa jimbo hilo Dr,Harrison Mwakyeme 2015.
Wazee hao walitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati
mwenyekiti huyo alipokuwa akitoa misaada ya kijamii katika tarafa hizo kama
moja ya kutimiza maombi ya misaada aliyoombwa na wananchi kwa ajili ya
kuondokana na changamoto zinazowakabili.
Jakson Mwakanyamale mkazi wa Ntebela alisema kuwa mwenyekiti
huyo amesaidia mambo mengi hasa sekta ya elimu,afya,kilimo na kuviwezesha
vikundi vya wajasilia mali na kuwa wao kama wazee wa Kyela wanamuhitaji ili awe
muwakirishi wao.
Mwakanyamale alisema kuwa wilaya ya Kyela ina wasomi wengi
ambao wananyadhfa kubwa serikalini na kwenye sekta binafsi lakini wamekosa
uzalendo wakulisaidia jimbo hilo ambalo limekuwa likipoteza sifa siku hadi siku
kutokana na kuwa na matatizo lukuki yasiyo tatulika.
Evansi Mwakalyobi mkazi wa Unyakyusa alisema kuwa kazi za kuondoa
changamoto za wilaya hiyo zilitakiwa zifanywe na mbunge lakini mbunge wao
amewasaliti hivyo wanamuhitaji mwenyekiti huyo kwa kuwa tayari amefanya mambo
makubwa na jamii inamtambua.
Alisema kuwa wananchi wanaoingia katika wilaya hiyo wakitokea
mikoani wanashikwa na butwaa wanapoliona jimbo hilo likiwa choka mbaya
ukilinganisha na jinsi Kyela ilivyo na wasomi wengi ambao wengine wanasifika
kwa uchapa kazi lakini wanakotoka kupo hoi.
Mwenyekiti mtendaji wa asasi hiyo Abraham Mwanyamaki ambaye
pia ni mjumbe wa mkutano mkuu Taifa na mlezi wa Chadema wilayani humo alipoulizwa
kuhusu suala hilo alisema kama chama chake kitampa ridhaa atafanya hivyo.
Alisema kuwa amekuwa akiulizwa na watu wa kada mbalimbali
kuhusu kugombea ubunge katika jimbo hilo pindi anapofanya kazi za kijamii
kupitia asasi wakitaka agombee lakini hakuweza kujibu na kuwa kama wazee na
wananchi kwa ujumla wataona anafaa basi hata kuwa na kinyongo.
Wilaya ya Kyela ni moja ya wilaya katika mkoa wa mbeya
inayosifika kwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato kama zao la kakao,mpunga,mawese
na vinginevyo ambavyo vinaingiza pato kubwa huku miradi ya maendeleo ikisuasua
mengine ikijengwa chini ya kiwango kutokana na kukosa wasimamizi makini.
No comments:
Post a Comment