Wednesday 6 May 2015

Serikali imebainisha sababu za kushindwa kufikia lengo la nne na tano la millenia la kupunguza vifo vya kinamama wajawazito.


Serikali imeshindwa kufikia lengo la nne na tano la millenia la kupunguza vifo vya kinamama wajawazito hadi kufikia mia moja na 93 kwa kila vizazi laki moja kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuwa na vituo vya afya hamsini tu nchi nzima kati ya vituo 600 vyenye uwezo wa kutoa huduma dharura ya upasuaji kwa mama mjazito.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mpango wa kutoa elimu ya  utabibu kwa njia ya mtandao kwa watoa huduma wa afya vijijini,waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt.Seif Rashid amesema kituo kimoja cha afya kinagharamu kati ya shilingi milioni 700 hadi bilioni 1 ili kiweze kutoa huduma ya upasuaji kwa mama wajawazito hivyo ni fedha nyingi zinahitaji kwa vituo vyote 600 vilivyopo nchni.

Mkurugenzi wa  shirika la kimataifa la  kusaidia serikali za mikoa kutoa huduma za dharura za uzazi-WORLD LUNG FOUNDATION-Dkt .Nguke Mwakatundu amesema lengo la kuanzisha mpango wa kutoa elimu ya afya kwa njia ya mtandao ni kusogeza huduma kwa wananchi na kusisitiza kuwa muda wa miaka minane zaidi ya shilingi bilioni 19 zimetumika kujenga vituo vya afya vijijini,kuweka vifaa vya upasuaji pamoja na kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya.

No comments: