Thursday 7 May 2015

Wakazi wa kata ya Misima wamuomba Rais Kikwete kufuta hati za umiliki ardhi walizopewa wawekezaji miaka 10 iliyopita.

Wakazi wa kata ya misima iliyopo wilayani handeni mkoani tanga wamemuomba mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr,Jakaya Mrisho Kikwete kufuta hati za umiliki ardhi zaidi ya hekta 200 walizopewa wawekezaji miaka zaidi ya 10 iliyopita kufuatia baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji kutumia ulaghai wa kuwachangisha wakazi wa eneo hilo fedha wakidai kuwa walinyang'anywa mashamba yao na kupewa mwekezaji watarudishiwa ili waweze kuendelea na kilimo kama ilivyokuwa awali.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliotishwa na chama cha dira ya mabadiliko nchini uliofanyika katika kata ya misima wilayani handeni baadhi ya waaathirika wa tatizo hilo wamesema baadhi ya viongozi wa serikali wamekuwa wakiwamegea ardhi baadhi ya wawekezaji wanaokwenda kuwarubuni wakazi waliopo sehemu ya vijijini kisha kupitisha muhtasari katika mazingira ya kutatanisha hatua ambayo inaweza kusababisha mapigano makubwa baina ya pande hizo mbili.
 
Awali naibu katibu mkuu taifa wa chama cha dira ya mabadiliko (ADC) Bwana Doyo Hassan Doyo amesema kulingana na mgogoro huo wananchi wakatae kuchangishwa fedha za ulaghai kwa madai kuwa watarudishiwa mashamba yao na kuuita kuwa huo ni utapeli kwa sababu anayeweza kufuta hati ya uiliki ardhi ni mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na wala sio mwenyekiti wa serikaloi ya kijiji.
 
Kufuatia hatua hiyo mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Bwana Said Miraji amesifu jitihada za mkuu wa mkoa wa tanga kwa kusuluhisha mgogoro wa ardhi uliokuwa umeanza kufukuta katika eneo la ambaoni jijini tanga ambapo mwekezaji anayemiliki hekta zaidi ya 100 alitii ushauri wa kiongozi huyo wa serikali kisha kuamua kuwamegea wakazi wake eneo la kilimo hivyo amemuomba mkuu huyo afanye jitihada za aina hiyo kwa wakazi wa kata ya misima ili kuepuka machafuko

No comments: