Na Editha Karlo
Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wakiwasili nchini kwa boti hivi maeneo ya Kibilizi, Mkoani Kigoma. Bado idadi yao haijafahamika kwani bado zoezi la kuwaandikisha linaelea katika eneo hilo.Ujio wa waomba hifadhi hawa unakuja kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Burundi ambayo yameshika kasi na kusababisha wananchi kuanza kukimbilia nchini Tanzania.
Burundi ilikumbwa na machafuko katika miaka ya nyuma na baadaye kuwa na amani lakini sasa inaingia katika mgogoro tena baada ya Rais wa sasa Pierre Nkurunzima kutaka kuwania urais kwa muhula mwingine.
Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wakijiandikisha mara baada ya kuwasili nchini Tanzania leo kwa boti
No comments:
Post a Comment