SPIKA wa
bunge mheshimiwa ANNE MAKINDA ameahirisha kikao cha bunge mpaka kesho saa tatu
asubuhi kutokana na msiba wa mbunge wa Geita Mjini DONALD MAX aliyefariki dunia
jana jijini Dar-es-salaam.
Akiahirisha
kikao hicho leo Spika MAKINDA amesema marehemu MAX alilazwa kwa muda mrefu
mpaka kifo kilipomkuta jana mchana.
Amesema
kwa mujibu wa kanuni za bunge zilizopo mwenzao anapotangulia mbele ya haki
kunakuwa hakuna kikao cha bunge kwa siku hiyo.
Spika
MAKINDA amesema kwa sasa bunge linaendelea kuwasiliana na familia kuona
taratibu zinavyoendelea lakini kwa taarifa za awali ni kwamba marehemu MAX
anatarajiwa kuzikwa siku ya jumamosi jijini Dar-es-salaam.
Kifo cha mbunge huyo kimefanya idadi ya wabunge
waliofariki katika bunge la 10 kufikia nane.
Aidha katika hatua nyingine Katibu
wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Amina Makilagi ametoa salamu
za rambirambi kufuatia msiba wa mbunge huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisi kwake mjini dodoam amesema msiba huo ni pengo kubwa kwa CCM,
watanzania, familia yake, wanageita na bunge kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment