Kutoshirikishwa kikamilifu kwa wadau na watumiaji wa rasilimali za maji nchini kumedaiwa kuwa ndiyo chanzo cha migogoro mingi ya watumiaji maji ikiwa ni pamoja na athali mbalimbali zinazosababisha kupungua kwa rasilimali hiyo na kukauka kwa baadhi ya mito.
Hayo yamesemwa na mkuregenzi msaidizi wa raslimali za maji kutoka
wizara ya maji Dokta George Lugomela wakati akizungumza mjini iringa na
wadau wa usimamizi wa raslimali za maji kwenye bonde la rufiji
linalijumuisha mikoa 11 nchini na kueleza kuwa kwa muuda mrefu serikali
haikuwa na mpango madhubuti unaosimamia raslimali za maji hali
iliyopelekea migogoro mingi na hata matumizi yasiyo endelevu.
Afisa wa maji bonde la rufiji Idris Msuya amese bonde hilo licha ya
kuwa na mabwawa ya kuzalisha umeme ya mtera na kidatu pia ni maarufu
kwa kilimo kutokana na kuwa na hali ya hewa inayostawisha mimea
mbalimbali na hivyo kuwa eneo muhimu kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo
hivyo uwepo wa raslimali hizo unahitaji mpango mahususi wa usimamizi wa
maji katika bonde hilo lenye ukubwa wa karibu kilometa za mraba laki
mbili.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilolo Seleman Mzee
aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa iringa katika mkutano huo wa wadau wa
maji uliolenga kujadili mpango wa usimamizi na uendelezaji raslimali za
maji ulioandaliwa na serikali kwa kipindi cha miaka mitano na kughalimu
kiasi cha dola bilioni moja nukta tano amesema mpango huo utaondoa
matumizi ya maji yasiyofuata utaratibu huku mwaandaaji wa mpango huo
Profesa Alice Georgakakos akisema kuwa mpango huo pamoja na mambo
mengine pia umeainisha changamoto na fursa zilizopo katika matumizi ya
raslimali za maji katika eneo husika.
No comments:
Post a Comment