Wednesday, 24 June 2015

Wakazi watanga kuchukua sheria mikononi dhidi ya wahalifu wanao kamatwa na kuachiwa bila kuchukuliwa hatua.


Wakazi wa mitaa tofauti iliyopo kata ya donge jijini tanga wamesema kuwa watachukua sheria mikononi dhidi ya wahalifu ambao wamekuwa wakikamatwa lakini baada ya siku kadhaa huachiwa huru kufuatia vitendo vya uvunjaji na uporaji wa mali kwa raia wema kuongezeka hatua ambayo inatishia usalama wa raia na mali zao.

Hatua hiyo inafuatia mtu mmoja ambaye jina lake halijatambulika kupigwa mawe kisha mwili wake kuchomwa moto na wakazi hao kwa madai kuwa yeye na wenzake watatu waliokimbia walikutwa wakivunja duka la mfanyabiashara mmoja katika mtaa wa INDIAN OCEAN na kufanikiwa kuiba mafuta ya kupikia aina ya sunola ambayo yalikutwa pembeni mwa mwili wa marehemu baada ya kuchomwa.
 
Akielezea tukio la uporaji lililofanywa siku moja baada ya zoezi la kumchoma moto mtu huyo anayedaiwa kuwa ni kibaka  makamu mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa donge Bwana. Michael Chauka amesema matukio ya uporaji yanafanywa kuanzia saa moja usiku kwa kupora simu za mikononi hasa kwa watu wa jinsia ya kike hatua ambayo imekuwa ikitishia hali ya uaslama kwa wakazi wake.
 
Kufuatia hatua hiyo kamanda wa polisi mkoani tanga kamishna msaidizi wa polisi zubeir mwombeji amekiri kuuawa kwa mtu huyo lakini bado wanalifanyia uchunguzi tukio hilo ili kufahamu chanzo cha mauaji na waliohusika kuchukua sheria mikoni waweze kuchukua hatua dhidi yao.

No comments: