Mkaazi
wa jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa
tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika
hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana.
Juma alinaswa jana ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.
Juma alinaswa jana ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.
Kukamatwa
kwa Juma kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka
huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari.
Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.

Baada
ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini
kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa
akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na
askari wa hospitali hiyo. Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na
Virusi vya Ukimwi (WAVIU), Shani Mwaruka alikiri kukamatwa kwa kwa
mtuhumiwa huyo.
Alisema, Juma alinaswa baada ya uongozi kupata malalamiko kutoka kwa watu waliokuwa wakihitaji huduma katika hospitalini hiyo.
Alisema tayari hospitali hiyo iliweka mtego imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.
Alisema tayari hospitali hiyo iliweka mtego imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.
Baadhi
ya watu waliodaiwa kuombwa fedha na daktari huyo feki, wamesema
aliahidi kuwatafutia kazi mbalimbali katika hospitali hiyo.
Nae
mwananchi aliyekwenda kupata huduma hospitali ya Amana Cecilia alisema
Agosti 9 mwaka huu, kijana huyo aliwaeleza kuwa kuna kazi katika
hospitali ya Amana na yeye kama daktari bingwa anayefanya kazi hapo
anaweza kuwasaidia.
“Alituambia
kuwa fomu zinatolewa katika hospitali ya muhimbili sh. 150,000 lakini
kwakuwa wao ni madakatari atatufanyia kwa sh. 100,000 tu. Tulichanga
fedha hiyo na ilifikia 800,000 tukampatia,”alieza Cecilia.
Aliongeza,Juni 19 mwaka huu aliwaita katika hospitali ya Amana ili kufanyiwa usahili lakini hakutokea na simu akawa hapokei.
Aliongeza,Juni 19 mwaka huu aliwaita katika hospitali ya Amana ili kufanyiwa usahili lakini hakutokea na simu akawa hapokei.
“Tuliamua
kuuliza kwa madakatari kama wanamfahamu lakini hakuna aliyemfahamu
ndipo tulipobaini kwamba tumetapeliwa na kuamua kufanya mtego kwa
kushirikiana na uongozi uliofanikisha kumnasa leo ,”alieleza.
No comments:
Post a Comment