TAARIFA KWA UMMA
Ofis ya-TAMISMI inapenda kuwajulisha
wananchi juu ya orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato
cha tano kwa awamu ya pili kwa mwaka 2017. Wanafunzi hawa wataanza
muhula wa kwanza na masomo tarehe 24 Agosti,2017, na hakutakuwa na
mabadiliko yeyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika
shule walizopangiwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti
hadi tarehe 08 Septemba 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti
,atakuwa amepoteza nafasi.
Mwanafunzi mara uonapo jina lako kwenye
tovuti ya ofisi ya Rais TAMISEMI kwamba umechaguliwa kujiunga na kidato
cha tano inabidi kudowlod fomu ya kujiunga na shule husika kwenye
mtandao..
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi awamu ya pili mwaka 2017
pamoja na fomu za kujiunga na shule (joining instructions) inapatikana
kwenye tovuti ya Ofisi Ya Rais TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na,
Katibu Mkuu
Ofisi Ya Rais-TAMISEMI
23 Agosti 2017
No comments:
Post a Comment