Mwanamke
mmoja amekutwa akiwa ameuawa na watu wasiyofahamika na mwili wake
kutupwa kwenye nyumba ambayo haijamalizika kujengwa (Pagala) huku akiwa
amefungwa kwenye mfuko wa sandarusi na kuzungushiwa nguo alizokuwa
amevaa.
Hayo
yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoani Mwanza, DCP Ahmed Msangi
na kusema tukio hilo limetokea tarehe 16.08.2017 majira ya saa 11:30
jioni katika mtaa wa Kitangiri kata ya Kitangiri Wilaya ya Ilemela
mkoani Mwanza.
DCP
Msangi amesema mwili wa marehemu uliweza kuonekana mahali hapo baada ya
watoto waliokuwa wakicheza eneo hilo kuona kifurushi kilichotupwa
kwenye Pagala ndipo walipotoa taarifa kwa mama yao na baadaye kutoa
taarifa kwa uongozi wa Mtaa pamoja na kituo cha Polisi.
Aidha,
Kamanda Msangi amesema mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote bali
uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wauaji walimuua kwa kumziba pumzi
kisha kwenda kumtupa kwenye Pagala eneo ambalo siyo rahisi mtu kupita.
Kwa
upande mwingine, DCP Msangi amesema upelelezi unaendelea wa kuwatafuta
watu waliyohusika na mauaji ya mwanamke huyo kwa namna moja ama
nyingine. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya
Bugando kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.
No comments:
Post a Comment