Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha taarifa zilizosambaa
mitandaoni kwamba imempa siku 7 Mbunge wa Singida Mashariki na
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu kuomba radhi kwa kupotosha
umma
Kwenye
ukurasa wa twitter wa msemaji wa serikali ametoa taarifa akisema kuwa
taarifa hizo si za kweli, kwani hata mtu aliyetumika kuandika hiyo
taarifa yupo msibani.
"Umma
unaarifiwa kuwa baada ya tamko la jana Serikali haijatoa tamko lolote
tena.Uzushi unaosambazwa mitandaoni Jumapili hii ni wa kupuuzwa,
taarifa inayosambazwa ni ya uongo kwa kuwa hata Dkt. Abbas anayetajwa
kusaini bado yuko likizo ya kufiwa. Hatua kali zitachukuliwa", aliandika twitter ya Msemaji wa serikali.
Hapo
awali kulikuwa na taarifa iliyosambaa ikionyesha imetoka serikalini,
ikimtaka Mh. Tundu Lissu kuomba radhi huku ikimpa siku 7 tu za kufanya
hivyo.
No comments:
Post a Comment