Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula
ameziagiza halmashauri zote kuwafikisha mahakamani na kuuza mali zao
wadaiwa wote sugu wa kodi ya ardhi ambao wana madeni ya muda mrefu.
Mhe.
Mabula ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kukagua mifumo ya
makusanyo ya kodi ya ardhi mkoani Geita mara baada ya kukuta majina 100
ya wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi ambao hawajalipa kodi kwa zaidi ya
miaka 10.
Mhe.
Naibu Waziri wa Ardhi alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa
Geita kuhakikisha wadaiwa hao wa muda mrefu wanaandikiwa notisi ya muda
wa siku 14 na wasipolipa ndani ya muda huo wafikishwe mahakamani bila
kuchelewa na kama wasipolipa basi mali zao zipigwe mnada.
Aidha,
Naibu Waziri huyo alitembelea eneo lenye viwanja vilivyowekwa mpango wa
matumizi bora ya ardhi katika wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita
ambavyo vimepangwa kujengwa ofisi za serikali, shule, hospitali, makazi,
maeneo ya kuzikia, na huduma nyingine za kijamii.
Naibu
Waziri alimtaka mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale kuhakikisha mji huo
unapangwa vizuri na kuwekwa miundombinu ya barabara, maji safi na taka
na umeme ili kuepusha migogoro ya ardhi ambayo mara nyingi huibuka
kutokana na wilaya kutokuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi ya muda
mrefu.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla
anaendelea na ziara yake ya mikoa ya kanda ya ziwa ambapo anataria
kufanya ziara Mkoa wa Shinyanga hasa katika wilaya za Kahama na
Shinyanga Mjini.

No comments:
Post a Comment