Hivi ndivyo alivyokutwa bwana Rajabu akimchuna mbwa
Wananchi na Nokia ringo mikonini ,wakimpiga picha bwana Rajab.
UKISTAJABU ya Musa utaona ya firauni, hali hiyo iliwatokea wakazi wa
Ubungo Kibangu pale mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Rajabu aliponaswa
na wananchi akimchuna mbwa.
Baada ya Rajabu kufumwa akifanya kitendo
hicho, alipewa kibano na wananchi wenye
hasira kali akakiri kwamba mbwa huyo alikuwa akimuandaa ili akamuuzee
kama mishikaki na supu kwa wateja wake.
Baada ya wananchi kumtilia shaka anapopata nyama ya
kuuza kutokana na hali yake ya kiuchumi kuwa duni, waliunda kikosi kazi
cha kumchunguza ndipo arobaini yake ikatimia.
Mtoa habari huyo
alisema baada ya wananchi kuchukizwa na kitendo hicho waliamua
kumfikisha kijana huyo Kituo cha Polisi cha Kibangu. “Kijana huyo
alipohojiwa na polisi alikiri kufanya biashara hiyo kwa muda mrefu,”
kilisema chanzo chetu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alisema kuwa taarifa juu
ya tukio hilo hajazipata na akaahidi kuzifuatilia na kusisitiza kuwa
kama ni kweli kijana huyo alifanya kitendo hicho atachukuliwa hatua za
kisheria.
No comments:
Post a Comment