KLABU ya Arsenal itaangalia uwezekano wa
kukamilisha usajili wa kipa namba wa Brazil na klabu ya Queens Park
Rangers, Julio Cesar baada ya Kombe la Mabara.
Arsene Wenger anataka kipa mzoefu atengeneze ushindani kwa Lukasz Fabianski na Wojciech Szczesny.
Mazungumzo baina ya wawakilishi wa Cesar
na viongozi wa Gunners tayari yamefanyika, lakini hayajamalizika kwa
kuwa kipa huyo yupo kwenye majukumu ya kimataifa.
Anayetakiwa: Julio Cesar anatarajiwa kujiunga na Arsenal kufuatia kushuka daraja kwa Queens Park Rangers
The Gunners sasa inatarajiwa kumaliza
dili hilo mara moja tu, baada ya kubainika Roma ya Italia nayo imeingia
kwenye mbio za kuwania saini ya Cesar.
Kipa huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye
yupo huru kuondoka Loftus Road kufuatia kushuka kwa QPR hadi
Championship, anataka kubaki London ambako amezoea maisha tangu awasili
msimu uliopita akitokea Inter Milan.
Na The Gunners - ambayo inatumai
kukamilisha pia usajili wa Gonzalo Higuain wiki ijayo, baada ya kocha wa
Real Madrid, Carlo Ancelotti kufungua njia kwa mshambuliaji huyo
kuondoka Hispania - inajiamini dili hilo litakamilishwa baada ya
Fainali ya Kombe la Mabara Jumapili.
Wenger alitaka kusajili kipa wa Stoke,
Asmir Begovic na wa Liverpool, Pepe Reina lakini, licha ya kuwa na fungu
la bajeti ya usajili la Pauni Milioni 70, kocha huyo wa Arsenal ameona
hana sababu ya kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kipa.
Mtu wa kwanza: Cesar amekuwa kivutio Loftus Road licha ya timu yake kuipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu
Rangers itasikiliza ofa ya kiasi cha
Pauni Milioni 2 kwa Cesar, wakati mshahara wake wa Pauni 70,000 kwa wiki
halitakuwa tatizo kwa The Gunners, ambayo imetuma waangalia vipaji wake
nchini Brazil kumuangalia Cesar anachokifanya katika Kombe la Mabara.
Pamoja na mpango wa kuwasajili Cesar na
Higuain, The Gunners pia wanataka kumsajili beki wa Swansea, Ashley
Williams na kiungo wa Everton, Marouane Fellaini. Lakini masuala ya
kifedha yanatia saka kama Arsenal itaweza kusajili wachezaji wote hao.
Hadi sasa, Arsenal imegoma kumpa
Fellaini mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki na pia imeshindwa kufika dau
la Pauni Milioni 24 za kumnunua.
Amekosekana? Arsenal linataka kuwasajili Marouane Fellaini na Ashley Williams (chini)
No comments:
Post a Comment