Saturday, 29 June 2013

MARC VIVIEN FOE PART 2: KITUO CHA SOKA ALICHOJENGA KIMEGEUKA KITUKO SASA - MAN CITY PIA WAMTOSA




Wakati michuano ya kombe la mabara 2013 yakiwa yanavuka hatua ya nusu fainali huko Brazil, miaka 10 iliyopita wakati kama huu michuano hiyo ilikumbwa na majanga.

On 26 June 2003, Marc-Vivien Foe alidondoka uwanjani wakati akiichezea timu yake ya Cameroon katika nusu fainali dhidi ya Colombia na pamoja majaribio ya kujaribu kumtibia, mchezaji huyo akiwa miaka 28 alifariki dunia muda mfupi baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo.

Miaka 10 baadae, ni huzuni kugundua kwamba kumbukumbu ya mchezaji wa zamani wa West Ham na Manchester City inaanza kupotea kwa kiasi fulani - 'legacy' yake imeanza kupotea.

Muongo mmoja baada ya kifo chake, Foe alikuwa na ndoto ya kuwafunza vijana wadogo wa kikameroon na wanasoka wa kiafrika.

Aliianzisha Marc-Vivien Foe Sport Complex, kituo ambacho kilijengwa nje kidogo ya maeneo ya mji wa Yaounde. Lakini kwa bahati mbaya kituo hicho sasa kipo kwenye hali mbaya
Sanamu lilojengwa nje ya sehemu ya kuingilia tayari limeanza kupata ufa, rangi iliyopakwa kwenye majengo ya kituo hicho imeshapauka, pia majengo hayo yakianza kuharibika. Kama hakuna jambo litakalofanywa kushughulikia kituo hicho, siku moja kitageuka kuwa nyumba ya kulala wahuni.

Leo hii kila kitu kipo katika hali mbaya ndani ya kituo hicho - hakuna madirisha, kuta zimejaa mavumbi na huku wadudu wakizidi kuzingira mazingira ya kituo hicho.

Sehemu ilipokuwa limejengwa bwawa la kuogelea, kuna maji machafu yaliyojaa kwenye bwawa hilo, maji yenye rangi ya kijani huku uchafu ukiwa unaelea, pia kuna takataka za plastic na miti mbalimbali. 
Bwawa la Kuogelea 
Kwenye sehemu ya kuchezea kama palivyo sehemu nyingine za Cameroon kuna undogo mgumu, uliochimbwa kutengeneza uwanja miaka kadhaa iliyopita, na nyuma yake uwanja huo kuna pori. 

"Marc angerakabti majengo na eneo hili la kituo, alikuwa na nia ya dhati katika kuwakomboa vijana wa Cameroon na wengine wote Afrika wanaopenda kucheza soka, lakini tangu kifo chake hakuna hata mmoja aliyechangia katika kukiendeleza kituo hichi," anasema kwa masikitiko Amougou Martin Foe baba wa marehemu.  

Miaka minne iliyopita, kulikuwepo na sherehe za kumbukumbu ya Marc katika kituo hicho huku mechi za soka zikichezwa, lakini hilo pia siku hizi halifanyiki. 
Mwaka huu, ilifanyika sala tu katika kaburi la Marc katika kukumbuka siku ya kufa. Shughuli nyingine zinazofanyika katika kumkumbuka kama maandamano, mbio za baiskeli, na michezo mingine yote imeghailishwa na serikali mpaka 27 Julai kutokana mikutano ya kisiasa. 
Hakuna program yoyote rasmi kutoka kwa serikali ya Cameroon. Ahadi zimekuwa zikitolewa kwa takribani miaka 10 sasa, lakini hakuna jambo lolote lilofanyika.

"Serikali haifanyi jambo lolote kama ilivyowahi kuahidi. Ahadi zao zimekuwa hazikamiliki. "Miaka 10 ni kama jana na bado tunaumizwa na kifo cha Foe. Kama Baba ni vigumu kusahau."

Bila kuwa na uwezo wa kifedha ni vigumu kutunza kituo cha Foe za michezo na Amougou Foe anahuzunika sana juu ya jambo hilo. 
"Wasiwasi wa Marc ulikuwa ni vipi kama angeshindwa kumaliza kujenga kituo hichi. Alikuwa anataka kuwafunza vijana wadogo soka lakinijambo hilo kwa sasa halifanyiki. Kama familia yetu ingekuwa na uwezo tungejaribu kufanikisha ndoto yake."

Pia inaonekana wachezaji wenzie wa Cameroon hawana mpango wowote wa kumuenzi 'Marco' kama walivyokuwa wakimuita wenyewe.
Amougou Foe anaamini wachezaji wenzie aliocheza nao wangeweza kufanya kitu kuhusu kituo hicho, ikiwa wangekuwa na nia ya kufanya hivyo kwa sababu baadhi yao wana vituo vya soka hata nje ya Cameroon. 
"Kama angetokea mtu akatengeneza sehemu ya kuchezea, na kuwachukua vijana na kuwafundisha lingekuwa jambo jema sana; matamanio yangu ni kituo hichi kuwa hai." alisema

No comments: