BAADA ya kumnasa Carlos Tevez kutoka
Manchester hadi Turin, Juventus sasa inataka kubeba nyota mwingine wa
City, beki Aleksandar Kolarov naye ahamie Italia.
kutoka Sportsmail iliandika
mapema mwezi huu kwamba Kibibi Kizee hicho kimefufua mpango wake wa
kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Serbia na sasa The Sun linaripoti
kwamba, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yupo njiani kwenda klabu
hiyo.
Uhamisho huo utamfanya aungane
mshambuliaji Muargentina, Tevez, ambaye alishikishwa jezi ya Juve jana
baada ya kukubali uhamisho wa Pauni Milioni 10 kutua kwa mabingwa wa
Serie A, ingawa atalazimika kutumikia adhabu ya kufanya kazi za kijamii
England kwa saa 250.
Amezungumza na Juve: Kolarov anaweza kuungana na Tevez (chini, kulia) Italia
Kolarov alisajiliwa kutoka Lazio kwa ada
ya uhamisho ya Pauni Milioni 16 miaka mitatu iliyopita, na City inaweza
kuwa tayari kumruhusu kurejea Italia kwa hasara ya Pauni Milioni 7,
kutokana na Gael Clichy kufanikiwa kuwa chaguo la kwanza katika beki ya
kushoto ya klabu hiyo.
"Nipo kwenye mawasiliano na Antonio Conte wa Juventus, hivyo tutaona kitakachotokea," Kolarov aliliambia The Sun.
"Nataka uhakika wa kucheza,".
Kibibi Kizee kipya: Tevez akipeperusha jezi yake mpya ya Juve kwa mashabiki mjini Turin jana
No comments:
Post a Comment