Watu tisa wamejeruhiwa baada ya gari
aina ya Costa ikitokea Mzumbe kuelekea mjini Morogoro kuacha njia na
kisha kupinduka katika eneo la Kasanga barabara kuu ya MorogoroIiringa.
kwa mujibu wa mashuhuda wameeleza
tukio lilivyotokea ambapo gari hiyo ilikua na abiria 25 wakitokea Mzumbe
kuelekea mjini Morogoro na ghafla gari liliacha njia na kisha kupinduka ambapo
majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Kwa upande wake dereva wa gari hilo
John Mahimbo akizungumza akiwa amelazwa
katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro chini ya ulinzi wa polisi amesema
chanzo cha ajali ni gari iligoma usukani na kuacha njia kisha kupinduka huku
msaidizi wa matron wa hospitali hiyo Teresia Lebulu amethibitisha kupokea
majeruhi tisa lakini katika hao saba wameruhusiwa na waliobaki ni wawili na
hali zao zinaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment