Wednesday, 24 June 2015

Uchumi wa Ugiriki bado ni kitendawili



Mawaziri wa fedha wa kanda wa umoja wa ulaya walioko mjini Brussels nchini Ubelgiji,wamehitimisha mkutano wao wa kuhusiana na mgogoro wa kiuchumi unaoikabili Ugiriki bila ya suluhu.

Waziri wa fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schaeuble amesema kwamba hakuna hatua yoyote iliyofikiwa tangu mwanzoni mwa wiki hii,hapo awali mawaziri hao wa kanda walitazama ombi la hivi karibuni la kuinusuru Ugiriki.

waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wanasema kwamba serikali ya mrengo wa kushoto ya Ugiriki imeweka bayana kuwa mfuko wa kimataifa wa misaada unaonekana kusisitizia suala la kupunguza matumizi kuliko kufikiria kuongeza kodi .

Naye waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amefungua mawazo yake kupitia mtandao wa twitter mara baada tu ya kuhitimisha mkutano baina yake na wakopeshaji ambao ameeleza kuwa wanaonekana kutokuwa tayari kutaka makubaliano,ama walikuwa wakijikuwadia kwa maslahi maalum katika Ugiriki .Na amehitimisha kwa kusema Athens inahitaji msaada wa kifedha ili kulipa deni inaloikabi mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi huu .

No comments: