Monday, 1 July 2013

Barack Obama ndani ya Tanzania



 a 038d1
s1.reutersmedia.net6 10156
s1.reutersmedia.net 7211c
Picha kwa hisani ya REUTERS
63dd79b1fa795515360f6a706700661b bc765
aa cfa09
cc 0f94a
dd 2cb9a
Picha Kwa hisani ya http://news.yahoo.com
 RAIS wa Marekani Barack Obama, amewasili nchini Tanzania katika mkondo wake wa mwisho wa ziara yake barani Afrika.
Ziara ya Obama inasemekana kulenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika.
Obama amewasili Tanzania baada ya ziara yake ya Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wa Tanzania kupitia mitandao ya kijamii wamekosoa ziara ya Obama katika nchi yao, wakisema kuwa ziara yake imeathiri shughuli za maisha yao ya kila siku.
Obama alitembelea Senegal kabla ya kupitia Afrika Kusini na kisha Tanzania ambako ziara yake ya Afrika inaishia kabla ya kurejea Marekani.

No comments: