KOCHA David Moyes ametambulisha benchi
lake la ufundi katika siku yake ya kwanza rasmi kuanza kazi Manchester
United yenye maskani yake Old Trafford.
Moyes ameungana na watu watatu aliokuwa
akifanya nao kazi Everton, Kocha Msaidizi, Steve Round, kocha wa kikosi
cha kwanza, Jimmy Lumsden na kocha wa makipa, Chris Woods.
Wanachukua nafasi za Mike Phelan, Rene Muelensteen - ambaye ameteuliwa kuwa Msaidizi wa kocha Guus Hiddink klabu ya Anzhi Makhachkala - na Eric Steele ambao wote wameondoka katika klabu hiyo kufuatia kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu uliopita.
Dawati la kazi: David Moyes ameanza kazi rasmi leo Manchester United
Moyes amesema: "Nimefanya kazi na Steve,
Chris na Jimmy kwa miaka kadhaa na ninafurahi wameamua kuungana nami
katika klabu hii kubwa.
Karibu: Moyes amekutana na wafanyakazi kadhaa katika siku yake ya kwanza makao makuu ya klabu yake mpya, Carrington
Hapa tunaenda: David Moyes amewasili Carrington katika siku yake ya kwanza rasmi kazini Manchester United
Anaingia: Moyes anakabiliwa na changamoto kadhaa katika mwanzo wake wa kazi United
Round, mwenye umri wa miaka 42, amefanya
kazi na Moyes tangu Julai 2008 wakati Woods amekuwa kocha wa makipa wa
Everton tangu 1998. Oktoba 2011 alikuwa kocha wa makipa wa Marekani.
Lumsden, mwenye umri wa miaka 65, amekuwa akifanya kazi na Moyes tangu akiwa Preston North End na tena Goodison Park.
Lumsden, mwenye umri wa miaka 65, amekuwa akifanya kazi na Moyes tangu akiwa Preston North End na tena Goodison Park.
Makamu Mwenyekiti wa United, Ed Woodward
amesema: "Nina imani na David na timu yake mpya katika nafasi hii, na
pamoja na benchi lake la ufundi la sasa, sasa tunaweza kuanza maandalizi
ya msimu mpya ujao,".
Kikosi: David Moyes akiwa katika picha ya pamoja na Kocha Msaidizi, Steve Round (kushoto) na kocha Jimmy Lumsden (kulia)
Moyes sasa anakabiliwa na mambo matatu makubwa, kwanza kutatua sakata la mshambuliaji Wayne Rooney anayetaka kuondoka, kufuatia kutofautiana na kocha aliyemtangulia, Sir Alex Ferguson.
Asiye na furaha: Rooney alisotea namba kikosi cha kwanza cha United msimu uliopita
Lakini pia Moyes anakabiliwa na changamoto ya kuboresha safu ya kiungo ya Manchester United kutokana na kiungo wa sasa Michael
Carrick kuonekana yupo katika kiwango cha chini na sasa Paul Scholes
amestaafu, huku Tom Cleverley na Anderson wakionekana kushindwa kutatua
tatizo hilo tu kwa kuandamwa na majeruhi na kushindwa kuwa wachezaji wa
uhakika katika kikosi cha kwanza.
Angalau Darren Fletcher ambaye ni
mgonjwa ameonekana kuweza jukumu hilo, wakati Phil Jones anaonekana
anafaa zaidi katika beki ya kati kuliko kiungo.
Tom Cleverley (kushoto) na Anderson wameshindwa kuwa wachezaji wa uhakika kikosini United
Anayetakiwa sana: Thiago Alcantara,
akiwa na Kombe la Euro 2013 kwa vijana chini ya umri wa miaak 21,
anatakiwa na United akaimarishe safu ya kiungo
Lakini pia kuna suala la wachezaji wa kuondoka, nalo pia ni jukumu la Moyes kuamua. Zaidi ya Rooney,
kuna wacehzaji wengine kama Nani - ambaye anatakiwa na Monaco na
Juventus - na Anderson aliyesainiwa kama chipukizi mwaka 2007, lakini
ameshindwa kuwa na maendeleo mazuri.
Katika ulinzi, Patrice Evra, mwenye
miaka 32 sasa, naye anatarajiwa kuhamia Monaco au PSG kufuatia habari za
United kutaka kumsajili Leighton Baines.
Ataondoka? Patrice Evra anaweza kuondoka United, hususan wakimsajili Leighton Baines wa Everton
No comments:
Post a Comment