Monday, 23 June 2014

HIVI NANI MWALIMU WA MAISHA BORA?...




Ni vyema kama ningemjua mwalimu wa maisha bora hapa nchini ingependeza ili nimuulize maswali haya
1.Nifanye nini ili watanzania waondoke kwenye wimbi la masikini
2.Umasikini unatokana na nini hapa nchini maana kuna kila rasilimali za kutufanya tuweze kufanikiwa
3.Ivi kwanini Tanzania kuna watu ni matajiri sana wa kawaida na wengine ni masikini wa kutupa
4Wewe mwalimu upo upande upi, Je Ni masikini, Tajiri au upo katikati.
Jamani hata kama Umaskini ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya binadamu ya msingi kama vile chakula, maji masafi, huduma za afya, mavazi na nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua. Hii pia inajulikana kama umaskini uliokithiri au ufukara. Umaskini wa kadri ni wa kuwa na raslimali chache zaidi au mapato madogo zaidi ikilinganishwa na watu wengine katika jamii au nchi au ikilinganishwa na hali ya kadiri duniani. Hali hii pia hujulikana kama umaskini halisi au unyonge. Umaskini linganishi ni hali ya kuwa na rasilimali chache au kipato cha chini kuliko wengine kwenye jamii au nchini, au ikilinganishwa na wastani duniani kote,, lakini hakuna jawabu la haraka kwanini Tanzania ni masikini.

No comments: