Kichanga
kinachokadilwa kuwa na umri wa miezi kati ya 6-7 kimekutwa kimetupwa
kwenye dambo karibu na mahakama ya mwanzo mkabala na ofisi za manispaa
ya iringa, mkoani iringa na mwanamke mmoja ambaye hakufahamika mara moja
leo. Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha
kuwepo kwa tukio hilo na kusema wanamtafuta mwanamke aliyefanya kitendo
hicho ili sheria iweze kuchukua mkondo wake pamoja na kukomesha vitendo
hivyo mara moja mkoani hapa. (FRIDAY SIMBAYA NA MARTHIAS CANAL)
No comments:
Post a Comment