Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shaarif Hamad ametangaza rasmi nia yake ya kugombea urais wa zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF katika uchagzui mkuu wa mwezi wa oktoba mwaka huu.
Maalim Seif ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho cha CUF ametoa msimamo huo nyumbani kwake mbweni baada ya kuwapokea uongopzi wa CUF waliongozana na wanchama wa wilaya ya mjini ambao walikwenda kumkabidhi fedha taslmu milioni 2 na nusu zikiwa ni za kumdhamni ili agombee urais wa Zanzibar ambapo amemesema pamekuwepo na maswali mengi kuhusu yeye kugombea nafasi hiyo hivyo uwezo anao na nia hiyi ipo.
Akizungumzia uchaguzi Maalim Seif amesema chama kimejindaa kikamilifu ambapo pia amesema endapo wazanzibar watampa ridhaa ya kuongoza serikali ya kitaifa atahakiksha seriklai yake inaweka misingi imara ya utawala na kujenga umoja na kuwa na uchumi imara.
Mapema mwenyekiti wa CUF Zoni ya mjini MASOUD KHAMIS amesema wao wamemamua kukusanya fedha hizo na kumtaka achukue fomu ya urais kwa vile wana imani naye na uongozi wa nchi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Maalim kudhaminiwa na wanachama wake huku kukiwa hakuna dalili yeyote ya kujitokeza mwanchma mwingine wa chama hicho kutaka kugombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha CUF.
No comments:
Post a Comment