Zaidi ya kaya 600 katika wilaya ya moshi mkoani kilimanjaro hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kujaa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku na kusababisha mafuriko ambayo yamevunja kingo za mto kikuletwa na kuelekeza maji yake katika makazi ya wananchi.
Wakizungumza kwa masikitiko wananchi hao ambao baadhi yao kwa sasa wamehifadhiwa katika nyumba za ibada ,shule na wengine katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha TPC wamesema kwa sasa wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana mali zao ikiwemo baadhi mifugo na vyakula kuchukuliwa na maji.
Wananchi hao wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia misaada ya haraka ya chakula na dawa kutokana kuwepo hatari ya kupatwa na magonjwa mlipuko na malaria.
kwa upande wake diwani wa kata ya TPC Bw.Rojas Mmari na afisa utala mkuu wa kiwanda cha kuzalisha sukari TPC BW.JAFARY ALLY wamesema kwa takribani miaka 30 kata hiyo haijawahi kukubwa na mafuko makubwa kamahayo na kwamba wananchi hao wanahitaji msaada wa haraka wa vyakula nguo na vyandarua.
Kufuatia tatizo hilo mbunge wa viti maalum chadema mkoa wa kilimanjaro Mh.Lucy Owenya ametembelea wananchi hao na kuona adha waliyoipata na kutoa msaada wa chakula ambapo ameitaka serikali ya wilaya kuchukua hatua za haraka za kusaidia wananchi hao.
No comments:
Post a Comment