Monday, 4 May 2015

Ofisi ya taifa ya Takwimu yasisitiza watendaji wa serikali kuanza kutumia Takwimu mpya kuwahudumia wananchi.


Kamishina wa sensa ya watu na makazi Bibi Amina Mrisho amezitaka mamlaka,taasisi za serikali na mashirika binafsi kuaanza  kutumia Takwimu mpya  zitakazo saidia katika utengenezaji wa bajeti mbalimbali na kurahisisha utekelezaji wa mipango ya serikali katika kuwa hudumia wananchi.

akizungumza wakati wa semina ya usambazaji wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyojumuisha wadau wa Takwimu na viongozi wa serikali ya mkoa wa Morogoro amewashauri watendaji kuanza kutumia Takwimu hizo kwani tayari ofisi ya taifa ya Takwimu imekwishaziweka kwenye tovuti na katika mitandao mbalimbali ambapo amesema usambazaji wa takwimu hizo umeanzia mkoa wa Morogoro  na badae zitasambazwa nchi nzima ili zianze kutumika.
 
Naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta. Rajabu Rutengwe amesema Takwimu hizo zitasaidia kupunguza migogoro ya mipaka kati ya wakulima na wafugaji hasa katika wilaya za kilosa na Mvomero endapo watendaji wa ngazi na vitongoji vijiji,kata watazitumia kwa usahihi na kwa watu sahihi bila kujali ukabila kwani Migogoro hiyo kwa muda mrefu sasa imegharimu maisha ya wananchi wengi.
 

No comments: