Madereva wa mabasi mkoani Arusha wamesema mgomo unaoendelea ni matokeo ya utendaji mbaya wa baadhi ya watendaji wa taasisi za serikali,na pia baadhi ya wamiliki ambao badala ya kutatua tatizo la msingi wamekuwa wakitupiana mpira na kuangalia maslahi yao huku wao wakiendelea kuteseka na kuebebeshwa mzigo wa lawama.
Wakizungumza katika kituo kikuu cha mabasi jijnini Arusha madereva hao wanasema wameshalalamika vya kutosha na hakuna kisichojulikana na wanashangaa kuona watekelazaji badala ya kushulikia tatizo la msingio wanaendelea kuwaongezea mzigo huku wakiwageuza kuwa mradi wao wa kiuchumi madai ambayo pia yanaungwa mkono na abiria.
Baadhi ya wamiliki wa mabasi mkoani Arusha na viongozi wa usafirishaji wa abiria akiwemo Bw.Adolf Loken ametolea ufafanuzi baadhi ya malalamiko ya madereva hao huku akidai kuwa baadhi yana msingi na mengine hayana msingi.
No comments:
Post a Comment