MAHAKAMA
ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora juzi ilitupilia mbali kesi tano
zilizokuwa zimefunguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi wa Serikali za
Mitaa uliofanyika Desemba 14, mwaka jana.
Kesi
hizo zilifunguliwa na CCM katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga Aprili,
mwaka huu, ambapo chama hicho kilikuwa kikipinga ushindi walioupata
wenyeviti watano wa Serikali za Mtaa, ukiwemo wa Stoo, Kamando,
Mwayunge, Nkokoto na Kijiji cha Simbo wilayani humo.
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Leonadi Nkola,
alisema madai yalitengenezwa na mtayarishaji mmoja, hivyo kila neno na
sentesi zilifanana na tofauti yake ni katika majina na katika makosa
yaliyofanywa baada ya uchaguzi, mawakala wao waliweza kusaini na
kukubaliana na matokeo kwa msimamizi mkuu wa Uchaguzi wa Wilaya na
kwenda kinyume cha sheria.
Aidha
Hakimu Nkolo alibainisha kuwa katika madai yao pia hawakuweza kuonyesha
barua yoyote ambayo walimwandikia msimamizi wa uchaguzi wa wilaya
inayopinga matokeo ya ushindi.
Akiendelea
kusoma hukumu hiyo, Nkola alisema katika hati hiyo ya madai
iliyoandaliwa haikuweza kutoa nukuu ya kifungu cha sheria
kinachothibitisha ukiukwaji wa uchaguzi huru na haki kwa kuvunja sheria
na kanuni za uchaguzi na kufanya madai yao kutokuwa ya msingi na sheria.
Kutokana
na kukosekana uthibitisho wa madai hayo, Mahakama ilitupilia mbali
madai hayo na kusema kuwa hao ni viongozi haramu wa Serikali za Mitaa.
Viongozi
wa CCM walioshindwa ni pamoja na Julius Mpuya Mtaa wa Kamando, Abeid
Issa wa Mtaa wa Nkokoto, Majenga Mashauri Mtaa wa Stoo, Ally Isike Mtaa
wa Mwayunge na Athuman Mohamed wa Kijiji cha Simbo,
Aidha
viongozi walioshinda upande wa Chadema ni Joseph Njile wa Mtaa wa Stoo,
Abel Shampinga Mtaa wa Mwayunge, Gerad Ndezi Mtaa wa Nkokoto, Julius
Kitundu Mtaa wa Kamando na Yusuph Finyongolo wa Kijiji cha Simbo.
No comments:
Post a Comment