Saturday, 27 June 2015

NEMC yawapiga marufuku wenyeviti wa mitaa kutoa vibali vya matumizi ya ardhi vinavyokiuka sheria.



Baraza la taifa la usimamizi wa mazingira limepiga marufuku wenyeviti wa mitaa kutoa vibali vya matumizi ya ardhi vinavyokiuka sheria za hifadhi ya mazingira ikiwemo ujenzi usiozingatia mifereji ya maji, hifadhi ya kingo za mito na bahari.

Akizungumzia hatua hiyo mwanasheria baraza la usimamizi wa mazingira NEMC Bw. Heche Suguta aliyefuatana na maofisa wa mipango miji manispaa ya Kionondoni ameeleza kusikitishwa na hatua ya mwenyekiti wa mtaa wa msasani bonde la mpunga ambaye hakuwepo katika eneo la tukio kutoa kibali cha kuchimba mtaro mkubwa wa kupeleka maji machafu baharini kinyume cha sheria.
 
Katika maagizo ya NEMC Bw.Suguta ameagiza mtaro huo kuzibwa ndani ya siku tatu kwa gharama yao wenyewe huku akipiga faini ya zaidi ya milioni mia moja katika viwanda vilivyo kiuka masharti ya mazingira na usalama kazini huku afisa mipago miji Bi.Juliana Nyaitara akieleza lengo la operesheni hiyo kuhakikisha manispaa ya kinondoni inafakiwa katika hufadhi na usafi wa mazingira.

No comments: