Wakulima zaidi ya laki saba kutoka mikoa ya mwanza,mbeya,Kilimanjaro na Iringa wanasadikiwa kuathirika na viwatilifu vyenye sumu kali vinavyotumika kuua wadudu na magugu mashambani kutokana na ukosefu wa elimu ya kujikinga na matumizi ya viwatilifu hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na kaimu msajili wa taasisi ya utafiti na
udhibiti wa viwatlifu nchini –TPRI- Dokta Elikana Lekei wakati akitoa
elimu juu ya matumizi bora ya kujikinga na madhara ya viwatilifu kwa
wakulima na wafanyabiashara wa dawa hizo katika wilaya zote za mkoa wa
Mtwara.
Amesema kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa mwaka 200-2006 katika
mikoa hiyo imeonyesha madhara ya viwatilifu ni makubwa nchini na mkakati
uliyopo hivi sasa ni kuangalia maeneo yenye athari kubwa ili wakulima
wapimwe lakini pia wapewe ushauri utakaosaidia kuwapunguzia matatizo ya
kiafya.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wakizungumzia hali hilo wamesema
elimu hiyo imewawezesha kutambua madhara ya viwatilifu hivyo hasa
vitumikavyo kwenye mmea wa mkorosho ambavyo vingi vinauzwa kiholela.
No comments:
Post a Comment