Chama
cha Demokrasia na mandeleo Chadema kimesema kita hakikisha kina pinga
vikali mswaada wa sheria wa vyombo vya habari unao tarajiwa kupitishwa
bungeni usipitishwe, kwasababu una lenga kukandamiza vyombo vya habari
vya watu binafsi.
Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa Singida
mashariki Mhesimiwa Tundu Lissu amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara
wilayani Ikungi, na kusema kuwa lengo la serekali ni kuwarudisha
watanzania miaka ya nyuma, ili kuweza kuficha maovu yanayo tendeka ndani
ya serekali kwa kutumia chombo kimoja cha taifa cha habari.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Tundu Lissu amewataka wananchi wa
jimbo la Singida mashariki kujitokeza kujiandikisha katika daftari la
wapiga kura kwa wingi, kwa kufanya hivyo watakuwa na nafasi kubwa ya
kushinda katika uchaguzi mkuu kama jinsi walivyo fanikiwa kushinda
katika uchaguzi wa serekali za mitaa kwa kupata ushindi wa zaidi viti
arobaini huku CCM ikiambulia viti tatu.
Akiongea na maelfu ya wakazi wa jimbo la Singida mashariki waziri
kivuli wa maliasili na utalii na mbunge wa Iringa mjini Mheshimiwa
mchungaji Peter Simioni Msigwa, amesema baadhi ya viongozi wa CCM wame
hujumu nchi kwa kutorosha maliasili nyingi hapa nchini, na kumekuwa na
rushwa karibu katika sekta zote hata kusababisha huduma muhimu kama
hospitali kukosa madawa, kutokana na hali hiyo Chadema imeamua kusimama
imara na kutembea nchi nzima kuwaeleza wananchi na ili waweze kujua
wachague chama gani katika uchagu mkuu unao kuja.
Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na mamia ya wakazi wa jimbo
la Singida mashariki wakiwemo wachungaji wa makanisa mbalimbali mashehe
na wananchi wa jimbo hilo wameonyesha niayao ya kumrudisha mbunge wao
kwasabau ya kuwatetea wananchi kuacha kuchangia michango maendeleo
ambayo inatakiwa kutolewa na serekali.
No comments:
Post a Comment