Monday, 1 June 2015

Wananchi wa Lekimurunyi wilayani Arumeru wadaiwa kufeka mazao ya kijiji jirani cha Olkung'wadu.


Mgogoro wa ardhi kugombea mpaka kati ya kijiji cha Olkung'wadu wilaya ya Arumeru na Lekimurunyi wilaya ya sia umeingia katika hatua ya uvunjifu wa amani baada ya watu wanaodaiwa kutoka kijiji cha Lekimurunyi wakiwa na silaa za jadi kuvamia kijiji cha Olkung’wado kufeka zaidi ya hekari thelasini za mzao ya mahindi na nyanya pamoja na kubomoa vibanda wanavyo ishi kwa muda wakiwa shambani.
Wakizungumza na ITV iliyofika katika eneo ilo na kushuhudia uharibifu uliyofanyika wakazi wa kijiji cha Olkugw’ado waliyo patwa na mkasa huo wamesema tukio ilo limefanywa usiku na kundi la watu waliyo ingia katika mashamba kuwakimbiza wakulima na kisha kufeka na kuharibu mazao hayo ambayo tayari yalikuwa yamekomaa.
 
Mwenyekiti wa kitongoji cha Orok mahali palipo fanyika uharibifu  Terewali Nko amesema wakazi wa eneo ilo wanaishi kwa mashaka makubwa kutokana na tishio la uvamizi wa kutumia silaa unatokea mara kwa mara na ameiomba serikali ichukue hatua.
 
Kwa upande wake mbunge wa Arumeru mashariki Joshua Nasari amesema anashindwa kuelewa kwanini serikali mbili za mkoa wa Kilimanjaro na Arusha zinashindwa kumaliza mgogoro huo wa muda mrefu na kwamba kuna kila dalili za kutokea kwa umwagaji wa damu kutoka na hali inavyo endelea lakini yeye anaendelea na juhudi za kumaliza mgogoro huo.

No comments: