Baadhi
ya wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya igunga wametishia kufunga
ofisi ya chama kushinikiza katibu wa CCM wilaya hiyo aondolewe kwa
madai ya matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo kufuja fedhazinazotolewa na
wadau kwa ajili ya kusaidia vijana hatua ambayo imesababisha mgawanyiko
mkubwa kwa wanachama hususani wakati huu mgumu wa kuelekea katika
mchakato wa uchaguzi mkuu.
Mapema asubuhi baadhi ya wanachama wazee na vijana wameonekana
wakiwa jazba ya kutaka kufunga ofisi huku wameshika mabango yenye ujumbe
mbalimbali wa kutaka uongozi wa juu kumuondoa katibu wa chama cha
mapinduzi wilaya ya igunga bw.abdallah kazwika,wakimtuhumu kutumia
vibaya madaraka yake.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya igunga Bi.Zipora Pangani
alifika katika ofisi za ccm ambapo kabla ya kusikiliza hoja na madai ya
wanachama hao alitoa amri kali ya kuwataka waondoke maeneo ya ofisi yao
hatua ambayo ilipingwa na wanachama hao huku walalamikia hatua ya mkuu
huyo wa wilaya kwamba ameingilia uhuru wa wanachama kwa kutumia nguvu ya
madaraka aliyopewa na serikali.
Hata hivyo jeshi la Polisi wilayani igunga lilitumia busara pasipo
kutumia nguvu kama ilivyozoeleka katika matukio mengine kuwatawanya
wanachama hao huku katibu wa ccm wilaya ya igunga Bw.Abdallah
Kazwika akipinga tuhuma hizo dhidi yake.
No comments:
Post a Comment