Gari lililoporwa likiwa na matundu ya risasi.
Polisi wakiwa eneo la tukio.
Mmiliki wa gari kushoto akitoa maelezo kwa polisi. (DK)
Askari wa usalama barabarani akilikagua gari.Polisi wakiwa eneo la tukio.
Mmiliki wa gari kushoto akitoa maelezo kwa polisi. (DK)
MAJAMBAZI
wanaokadiriwa kuwa watatu leo mchana wamefanya uporaji kwenye maduka
matatu ya kutoa na kuweka fedha kwa njia ya simu maeneo ya Mikocheni
Kwa-Mwalimu Nyerere jijini Dar ambapo baadaye walitoroka na wawili kati
yao kukamatwa.
Mashahidi
waliokuwepo aneo husika walisema baada ya uporaji huo, majambazi hao
walipora gari aina ya Suzuki-Vitara na kuondoka nalo lakini walipofika
mita chache karibu na baa maarufu ya Rose Garden, gari hilo liliwagomea
kwenda na kuanza kupiga king’ora cha hatari (alarm) kitendo
kilichowafanya washuke na kuanza kutafuta njia nyingine ya kujiokoa
ambapo aliyeshika ‘fuba’ la fedha alifanikiwa kupora pikipiki aina ya
Boxer na kutokomea na wawili waliokuwa wakitafuta njia ya kujinasua
walitiwa mbaroni na askari polisi waliokuwa wakiwafukuza.
No comments:
Post a Comment