Viongozi wa vyama vya kisiasa, maafisa uandikishaji na kamati za ulinzi na usalama wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera zimekili kushindwa kudhibiti wimbi la watu wanaosadikiwa kuwa wahamia haramu kutoka nchi ya Burundi, Rwanda na Uganda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura BVR wakishawishi baada ya watendaji wa serikali za vijiji, vitongoji na mawakala kuwapatia rushwa ya fedha na mifugo.
Wamebainisha hayo siku chache baada ya kukamilika kwa zoezi la
uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura BVR katika mkoa wa
Kagera ambapo wilaya ya Kyerwa imevuka lengo kwa kuandikisha watu wengi
zaidi wakiwemo wahamiaji haramu zaidi ya 4000 huku wilaya ya Karagwe
ikiandikisha kwa asilimia 97 na kubainisha kwamba wahamiaji haramu
walioweka makazi katikati ya mapori na misitu ya hifadhi ya taifa
walivamia zoezi la BVR kwa lengo la kujiandikisha kinyume cha sheria za
nchi.
Baadhi ya wanasiasa wamesema kuwa wimbi la wahamiaji haramu katika
wilaya zilizopo mipakani halitaisha endapo serikali isipobadilisha mfumo
wa utendaji katika maeneo ya mipaka ya nchi ambapo takwimu zinaonyesha
kila siku wilaya ya Kyerwa na Karagwe watu 30 kuingia nchini kwa njia za
panya.
Wakijibu malalamiko hayo kaimu mkuu wa wilaya ya Kyerwa Bw.
Josephat Kakuru amesema kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu
12128 waliohifadhiwa katika kijiji cha Katera na Kihinda kwa lengo la
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
No comments:
Post a Comment