Sakata la migogoro ya vyuo vikuu vinavyodaiwa kutokuwa na usajili au kutokidhi viwango vinavyotakiwa limeibuka tena bungeni ambapo baadhi ya wabunge wameitaka serikali kuvifungia kwani licha ya kuwapotezea muda wanafunzi vinawatia hasara wazazi na serikali inayotoa mikopo kwa wanafunzi hao.
Hayo yameibuka bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali
na majibu ambapo baadhi ya wabunge wameihoji serikali kwa nini
inaendelea kuviachia vyuo hivyo viendelea kutoa huduma ambayo mwisho wa
siku inaitia hasara taifa kikiwemo chuo cha st joseph ambacho kinadaiwa
kutokuwa na usajili na chuo cha kampala ambacho hakina usajili wa bodi
ya famasia.
Akijibu maswali hayo naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mh
Janesta Muhagama mbali na kukiri uwepo wa vyuo ambavyo havifuati
taratibu za nchi amelihakikishia bunge hilo kuwa serikali inafanya
utafiti wa kina kwa kushirikiana na kamati ya huduma za jamii na
kuongeza kuwa vyuo vitakavyobainika hatua zitachukuliwa.
Suala la uhaba wa nishati ya mafuta nchini nalo likaibuka ambapo
mbunge wa Ubungo John Mnyika amewasilisha hoja ya dharura bungeni ili
wabunge waweze kujadili suala hilo liweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka
kabla madhara hayajawa makubwa.
Hata hivyo hoja hiyo haikuweza kuendelea kujadiliwa na wabunge
baada ya naibu spika Mh Jobu Ndugai kuwahidi wabunge hao kuwa endapo
tatizo hilo halitapatiwa ufumbuzi mapema mjadala utaruhisiwa huku
serikali ikikanusha kutokuwepo kwa uhaba wa mafuta na kwamba yapo ya
kutosha, na kutoa onyo kwa wenye vituo vya mafuta ambao wameyaficha kwa
madai ya kusubiri bei mpya.
No comments:
Post a Comment