Tuesday, 30 June 2015

Hali ya upatikanaji wa mafuta yazidi kuwa tete nchini.


Licha ya tamko la serikali la kuwataka wafanaybiashara wakubwa wa mafuta kuuza nishati hiyo lakini bado hali imeendelea kuwa tete baada ya vituo vingi kugoma kuuza nishati hiyo muhimu.

Ni dhahili kauli iliyotolewa na maafisa wa mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji ya kuwataka wafanyabiashara wakubwa kuachana na kilichoitwa ni mgomo baridi wa kuuza nishati hiyo huku wakisubiri ujio wa bei mpya ni kama imepuuzwa ambapo ITV imeshuhudia vituo vingi vya mafuta vikiwa vitupu huku vingine vikidiriki kuuza mafuta hiyo kwa uficho mithili ya magendo vile kwa kuruhusu gari mojamoja kuingia kwenye vituo hivyo.
 
Bw Tino Mmassy ni katibu mkuu wa chama cha wauzaji wa mafuta rejareja ambapo anasema wao wako tayari kuuza mafuta lakini wanakwamishwa na makumpuni makubwa ambao wamegoma kuwauzia huku mwenyekiti wa chama hicho akisema watahakikisha wanatumia mgogoro huu wa sasa kwakuhakikisha jambo hili kamwe halijirudii.
 
Ukosefu wa mafuta kwa siku kadhaa unatajwa kusababishwa na baadhi ay makumouni makubwa takribani 10 ya uuzaji wa mafuta kushindwa kuuza bidhaa hiyo kwa kile kinachodaiwa wanasubiri kuanza kwa bei mpya ya nishati hiyo pindi utakapoanza mwaka mpya wa fedha yaani julai mos mwaka huu.
 

No comments: