Mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi kuanzia shule ya awali hadi
darasa la saba Bi. Nazal Abraham anasema miundombinu ya shule hiyo ni
chakavu kwa madai kuwa shule hiyo ilijengwa tangu mwaka 1930 hadi sasa
haijafanyiwa marekebisho licha ya wanafunzi wanendelea kutumia madarasa
hayo.
Amesema walimu wanalazimika kutumia vyumba vitatu vyenye ufa
ambavyo vimebaki kufundishi wanafunzi hao kwa awamu hali inayosababisha
elimu inayotolewa kutokidhi viwango kutokana mazingira magumu ya
kufundishia.
Kutokana na tatizo hilo mamlaka ya elimu nchini (TEA )imetoa msaada
wa shilingi milioni 30 pamoja na kuendesha harambee iliyofanikisha
kupatikana kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 83.5 kwa ajili ya
ujenzi wa shule hiyo ambapo mkurugenzi wa ukuzaji raslimali kutoka tea
Bi. Silivia Lupembe anasema mazingira wanayosomea wanafunzi ni hatari.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya same Bw.Herman Kapufi ambaye
aliongozana na wadau mbalimbali kutembea shule hiyo amesema msaada wa
haraka unahitajika huku baadhi ya wanafunzi wakielezea changamoto
zinazowakabili ikiwemo uhaba wa vyoo na walimu.
No comments:
Post a Comment