Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini kamanda Mohamed Mpinga
ameyasema hayo alipokuwa akikabidhiwa gari maalum litakalotumiwa na
kikosi cha usalama barabarani katika utoaji wa elimu kwa watumiaji wa
barabara kwa ufadhili wa watu wa China kwa kushirikiana na ubalozi wa
China nchini Tanzania kupitia kampeni ya usalama wa barabarani
ujulikanayo kama endesha kwa usalama.
Zoezi hilo lilifwatiwa na zoezi la utoaji wa vyeti kwa madereva wa
pikipiki walio fuzu mafunzo maalum ya usalama barabara huku baadhi yao
wakisema ukosefu wa elimu na kutokujitambua kwa baadhi ya madereva
kunasababisha ongezeko la ajali hizo.
No comments:
Post a Comment