Monday, 22 June 2015

Shambulizi lawaua watu 4 Burundi



Polisi nchini Burundi wanasema kuwa watu wanne wameuawa na wengine karibu 30 kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya guruneti Jumapili usiku.
Mashambulizi hayo yalifanyika katika miji mitatu ukiwemo mji mkuu Bujumbura.
Polisi wanasema kuwa guruneti hizo zilirushwa na wafuasi wa upinzani ambao wanataka kuvuruga uchaguzi mkuu unaokuja.
Siku ya ijumaa watu 11 walijeruhiwa kwenye misururu ya mashambulizi ya guruneti.
Burundi imekumbwa na ghasia zilizoendeshwa na wapinzani wa rais Nkurunziza wanaopinga uamuzi wake wa kugombea urais kwa muhula wa tatu.

No comments: