Monday, 13 June 2016

Polisi Wamhoji Zitto Kabwe Kwa Dakika 90

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe  asubuhi ya leo June 13 2016 alikutana na wanahabari na kuzungumzia kuhusu polisi kuzuia kongamano ambalo liliandaliwa na chama hicho ili kujadili bajeti. Pia alizungumzia kuhusu yeye kusakwa na polisi kwa kuviziwa na sio kwa utaratibu wa wito.

Leo jioni  Zitto Kabwe alipokea wito wa kuhitajika Central polisi kwa mahojiano ambayo yalichukua zaidi ya dakika 90 .

Baada ya  kutoka kwenye mahojiano aliyepata nafasi ya kuzungumza ni wakili wa chama hicho Steven Mwakibolwa ambaye ameeleza sababu za wito huo kituoni hapo.

"Wamechukua maelezo ya Zitto kufuatana na kongamano la chama lililokuwa limezuiliwa jana.Baada ya mahojiano na mazungumzo na polisi, chama kitatoa taarifa rasmi juu ya nini kitafuta baada ya hapa."Amesema Mwakibolwa

"Kama alivyoeleza mwanasheria tumemaliza mahojiano na polisi kwa hiyo kesho tutatoa kauli yetu ya hatua inayofuata, nimeitwa polisi nimekuja, wanachama watulie tunaendelea na majadiliano na polisi ili tuendelee na kazi zetu za kisiasa kama kawaida" Amesema Zitto Kabwe

No comments: